Miujiza ya Ivory Coast hadi ubingwa Afcon

Baada ya hatua ya makundi mwenyeji alikuwa na hatihati ya kuendelea kuwepo kwenye mashindano katika ardhi ya nyumbani ilihitaji dua na kudra za Mungu kundi F lisitoe best looser na ikawa hivyo Zambia wakapoteza kwa Morocco ndio ukawa ufufuo mwenyeji akapata nafasi kufuzu hatua ya 16 bora.

Warumi 14:8 “Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”.

Wakati michunao inaanza hakuwa na umaarufu huu alionao kwa sasa Emerse Faé ni kama aliamua kuishi na Bwana akapitia mateso ya Goligotha akafa na siku ya 3 akafufuka akachukua jukumu la kulibeba Taifa lake kama Kocha wa muda akipokea timu kutoka kwa Jean-Louis Gasset na mwisho ametwaa ubingwa wa AFCON

Ufufuo ukaendelea kwa Sebastian Haller alilala kitandani zaidi ya siku 600 akipigania maisha yake baada ya upasuaji wa kutibu saratani ya korodani iliyokuwa ikimtafuna ni kama alipiga hodi kuzimu alafu mlango haukufunguliwa akarudi duniani na kupata nafasi nyingine ya kuishi.

Alianza mashindano akiwa na majeraha na kukosa michezo ya awali kwenye makundi ila mabao yake kuanzia hatua ya mtoano yamekuwa ya ushindi dhidi ya DR Congo kwenye nusu fainali na kisha Nigeria kwenye fainali

Toto Tundu Simon Adingra ni yule muhitimu wa chuo aliyepata kazi siku chache baada ya kuhitimu aliwasili Abdijan na majeraha akakosa baadhi ya michezo kwenye hatua ya makundi ila balaa lake likaanza hatua ya mtoano na kama unahisi ushawahi kuwa na siku mbaya jipe muda kumfikiria Ola Aina mateso, masimango maudhi kutoka kwa Adingra

AFCON hii ya 2023 imetoa somo hakuna mkubwa wala mdogo Cape Verde Angola Mauritania Equitorial Guinea Afrika Kusini wametoa mateso kwa vigogo wa soka Barani Afrika Algeria Egypt Cameroon Morocco Senegal zote hazikuvuka hatua ya 16 bora

Haller anatukumbusha tukifa tufe kwa bwana na tukiishi tuishi kwa Bwana chochote unachopitia usikate tamaa hakuna anaye fahamu kesho yajayo ni fumbo kesho ni nafasi nyingine ya kubadili hatma ya maisha yako

🇨🇮 Côte d’Ivoire wametawazwa Mabingwa wa Afrika kwa mara ya tatu katika historia yao Ubingwa uliojaa machozi jasho na damu simulizi halisi ya ukombozi.

Habari Zifananazo

Back to top button