Mjumbe CCM: Tunaenda kugombea sio kugombana

ARUSHA: MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa (CCM), Namelock Sokoine amesema kuelekea uchaguzi mkuu watu wanapaswa kufahamu  wanaenda kugombea sio kugombana.

Namelock ameyasema hayo leo akiwa jijini Arusha wakati wa kumpokea mjumbe huyo aliyeteuliwa na Rais Samia Hassan Suluhu kwenye nafasi hiyo ya wajumbe 28 wa Kamati Kuu ukumbi wa CCM Mkoa.

“Tusiumizane katika chaguzi tupo viongozi hapa ambao tutashiriki katika nafasi za ndani katika michujo tusitumie nafasi zetu kukanyaga wenzetu ambao hawapo katika vikao hivyo, namshukuru Rais Samia kwa kuniteua katika nafasi hii”

Amesisitiza kutoumizana katika uchaguzi huu mkuu wa mwaka 2025 badala yake viongozi wanaoshiriki kuamua katika maamuzi watende haki

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Thomas ole Sabaya ammpongeza Namelock kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo ya kuamua maamuzi ngazi za juu na kuongeza kuwa Rais Samia anatoa fedha nyingi mkoani Arusha kwaajili ya miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesisitiza amani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuongeza kuwa uchaguzi si kabila wala dini ya mtu bali ni uwezo wa kuchagua mtu mwenye kutatua changamoto.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button