Mjumbe Moro aipongeza CCM Ilani bora 2025

DAR ES SALAAM: MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Morogoro Mjini, Dk Ally Simba amekipongeza chama hicho kwa kuandaa Ilani  bora ya uchaguzi inayojali maslahi ya wananchi wake na taifa kwa ujumla na kwamba itakipatia chama hicho ushindi wa kishindo.

Hivyo, ameshauri wanachama wa CCM kuisoma kwa undani na kuielewa kikamilifu pamoja na kuitangaza  hususani wakati huu wanapoelekea  kwenye  uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Dk Simba  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano la Afrika Mashariki  amesema Ilani hiyo ya mwaka 2025-2030, imebeba matumaini makubwa kwa maendeleo ya taifa kutokana na  ubunifu wa kuweka vipaumbele vya kila mkoa.

Amesema kimsingi nguzo kuu za Ilani mpya ya mwaka 2025–2030 inajengwa kwa misingi ya mageuzi ya kisasa ya uchumi jumuishi, shindani na unaotegemea kuongeza thamani ya rasilimali za ndani huku ikiongeza fursa za ajira kwa vijana, kuongeza kipato cha wananchi na kupunguza umaskini.

Kazi na dawa mkutano CCM

“Hii ni dira yetu ya kisiasa,  tunapaswa kuilinda kwa hoja, shauku na unyenyekevu wakati wa kampeni.Tuanze Kujipanga kwa utekelezaji wake, wana CCM tuna kila sababu ya kuamini kuwa kwa ilani hii, Mgombea wetu wa nafasi ya Urais, Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Dk Emmanuel  Nchimbi wataibuka na ushindi wa kishindo” amesisitiza.

Pia amesema ilani hiyo  imezingatia kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii kwa kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji sambamba na kukuza matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi huku ikidumisha demokrasia na utawala bora.

Ameongeza ilani inagusa mahitaji ya kila mwananchi na kuakisi falsafa ya Rais Samia ya “Kazi na Utu” ikimuasa kila mtu kufanya kazi kwa kuheshimu na kuthamini utu wa kila mmoja.

Amesisitiza  kwa kiasi kikubwa,  Rais Samia  alianza kujenga urithi huo kwa vizazi vijavyo akiwemo binti yake Rafat (11) ambaye ameandika kitabu   kinachoitwa “The First Female President”, akihamasishwa na utendaji na uongozi wa Rais Samia.

“Nilijiuliza nini kilimvutia sana binti yangu na kwamba aliona nini ambacho mimi sikukiona..?,  ila baada ya kuhudhuria kwa siku mbili Mkutano Mkuu Maalum wa CCM jijini Dodoma, na kushuhudia uzinduzi wa Ilani, nilielewa vyema nini tafsiri ya kilichokuwa katika akili na fikra za binti yangu” amesema Dk Simba.

Ameeleza  ujasiri, uwazi na hekima ya kitaifa ya Dk Samia Suluhu Hassan inamfanya kuwa zaidi ya muhamasishaji na mbadilishaji wa mustakabali wa taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button