Mkakati maalumu kuwanasa wauguzi jeuri

GEITA: SERIKALI mkoani Geita imetangaza mpango rasmi wa kupokea taarifa za wauguzi na watumishi wa afya wanaofanya vitendo visivyo vya kiungwana kwa watu wanaohitaji huduma ya matibabu.
Mpango huo pia unahusisha upokeaji wa taarifa za watoa huduma wanaokaidi kwa makusudi sera ya huduma bure kwa watoto, wajawazito na wazee kwenye vituo vya huduma za afya.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dk Omari Sukari ametoa taarifa hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa alipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya cha kijiji cha Msangila wilayani Bukombe.
Dk Sukari amesema ili kufanikisha hilo, kila kituo cha kutolea huduma za afya kitabandikwa eneo la wazi namba za mawasiliano za Mganga Mfawidhi wa eneo husika na Mganga Mkuu wa Mkoa.

Amesema hatua hiyo itasaidia kila mtu anayehitaji huduma anapokutana na kadhia ya makusudi inayosababishwa na jeuri ya mtoa huduma basi atoe taarifa mara moja kwa viongozi hao.
Dk Sukari amewataka watumishi wa afya kuendelea kuishi kiapo cha kazi na maadili kwa kuwatendea haki na kuwahudumia wagonjwa bila ubaguzi na unyanyasaji wa aina yeyote.
Ameongeza pia watumishi wa afya wanapaswa kuzingatia sera ya afya inayoelekeza huduma bure za matibabu kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee wasiojiweza.
βHalmashauri tuendelee kuwafikia wazee hawa walio katika kundi hilo ili waweze kupata vitambulisho vya kupata huduma za matibabu bureβ, amesema Dk Sukari.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuona uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya unaendana na ubora wa huduma hizo.
Aidha akizungumza katika kijiji cha Bulega Shigela alipiga marufuku watoa huduma za afya kuwatoza wajawazito na kuwataka kina mama kutoa taarifa mara moja wanapopata kadhia hiyo.
Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Uyovu, Dk Timotheo Masota amesema ujenzi wa kituo cha Afya Msangila unagharimu sh milioni 689 kutoka Benki ya Dunia (WB) ili kusogeza huduma za afya.
Dk Masota amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 90 ambapo pia wamepata nyongeza ya sh milioni 238 kutoka WB kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi.




β 彑[ππππ ππππππ π ππ ππππ ππππ ππππππ ππππ]彑β
I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35,000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my lifeβ¦ This is what I do, check it out by visiting Following Linkβ¦
.
You can check moreβ¦β¦β¦β¦β¦β¦ https://Www.Payathome9.Com
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do…..Β Β Β https://www.work27.info