Mkataba huu una ukomo ila..

“Kuhusu muda, Mkataba huu utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi. Msingi wa Mkataba huu kuendana na mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa mikataba hiyo nchini.

“Iwapo Mkataba huu utakuwa na ukomo kabla ya kuisha mikataba ya miradi iliyo chini ya Mkataba huu, utekelezaji wa mikataba ya miradi baada ya kuisha kwa mkataba huu itakuwa batili.

Vile vile, uhai wa Mkataba huu utawezesha kuingiwa kwa mikataba mbalimbali yenye masharti na muda wa ukomo tofauti na ambayo yote inategemea msingi wa uhai wa mkataba huu.

Hivyo, endapo upande mmoja wa mkataba huu utajitoa, athari yake ni kufa au kuvunjika kwa utekelezaji wa mikataba yote ya miradi iliyoanzishwa chini ya Mkataba huu…,” amesema Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Bungeni Jijini Dodoma akiwasilisha Azimio la kuomba bunge kuridhia Mkataba kati ya Tanzania na Dubai.

Habari Zifananazo

Back to top button