Dk Mecktridis ahamasisha kilimo cha kisasa

Asisitiza elimu kutolewa zaidi kwa wakulima

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Malinyi, Dk. Mecktridis Mdaku, ameiomba Serikali kuchukua hatua za makusudi za kuboresha Sekta ya kilimo wilayani humo, akisisitiza kuwa maboresho ya miundombinu na upatikanaji wa ardhi ndiyo suluhu ya kuinua uchumi wa wakulima wadogo na wa kati.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma, Dk. Mecktridis amebainisha kuwa licha ya juhudi za Serikali, bado kuna vikwazo vinavyochelewesha tija inayokusudiwa kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.

Katika mchango wake, Dk. Mecktridis ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi wa umwagiliaji katika Kata ya Itete, lakini ametahadharisha kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto ya barabara mbovu za kufika mashambani na mifereji isiyokidhi mahitaji.

Amemtaka Waziri wa Kilimo kutenga bajeti mahususi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu inayozunguka mradi huo, ili kuwawezesha wakulima kufika masokoni kwa urahisi na kuongeza thamani ya mazao yao.

Aidha, Mbunge huyo amekumbushia utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji katika maeneo ya Usangule, Sofi, na Mtakasisi ambayo yamo ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesisitiza kuwa wananchi wa maeneo hayo wana matumaini makubwa na ahadi hizo, hivyo ameiomba Serikali kutoa ratiba rasmi ya kuanza kwa miradi hiyo pamoja na kutoa fedha za awali ili kuanza utekelezaji wake kwa vitendo bila kuchelewa zaidi.

Kuhusu changamoto ya ardhi, Dk. Mecktridis ameeleza masikitiko yake juu ya uhaba wa maeneo ya kilimo wilayani Malinyi, kutokana na sehemu kubwa ya ardhi kuchukuliwa na hifadhi.

Ameiomba Serikali kufanya mapitio ya haraka ya matumizi ya ardhi ili kupata uwiano sahihi utakaowawezesha wakulima kupata maeneo mapya ya uzalishaji, akisema kuwa bila ardhi ya kutosha, mapinduzi ya kilimo yataendelea kuwa ndoto kwa wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

Vilevile,amezungumzia mfumo wa Stakabadhi Ghalani akibainisha kuwa Jimbo la Malinyi lina jumla ya AMCOS 22, lakini bado wakulima wanakabiliwa na ucheleweshwaji wa malipo na kukosekana kwa mfumo thabiti wa kuwapatia wakulima malipo yao kwa wakati. Mfumo uliopo hauwapi wakulima manufaa wanayostahili.

Amependekeza kuanzishwa kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Malinyi chenye nguvu na uwezo wa kusimamia maslahi ya wakulima wake, ili kuwapunguzia wakulima adha ya kutegemea Vyama vya Ushirika vya Wilaya jirani za Ulanga na Kilombero, jambo ambalo ameliita kuwa si rafiki wala endelevu.

Aidha,amesisitiza na kuonesha umuhimu wa Serikali kuboresha mfumo wa Stakabadhi ghalani kwa kuufanya uwe wa kisasa zaidi, na wenye uwazi unaolipa wakulima kwa wakati, Mkulima akilipwa kwa wakati ataongeza uzalishaji na kuchangia zaidi katika uchumi wa Taifa.

Katika hatua nyingine, Dk. Mecktridis amegusia umuhimu wa upatikanaji wa mitaji na pembejeo, ambapo ameeleza kuwa wakulima hususani wa Malinyi wanashindwa kumudu gharama za uzalishaji kutokana na ukosefu wa mikopo nafuu, pembejeo kuchelewa kufika maeneo husika pamoja na huduma duni za ugani.

Ameiomba Serikali kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima katika Taasisi za kifedha, pamoja na kuboresha usambazaji wa pembejeo kwa wakati.

Aidha, Maafisa Ugani waongezewe na wawezeshwe ili waweze kuwafikia wakulima vijijini na kuwapa elimu ya Kisasa ya Kilimo.

Ameeleza kuwa wakulima wengi wanashindwa kumudu gharama za uzalishaji, hivyo kuna haja ya kuimarisha huduma za ugani na kuhakikisha Maafisa Ugani wanawafikia wakulima vijijini kuwapa elimu ya teknolojia ya kisasa ya kilimo.

Akihitimisha mchango wake, Dk. Mecktridis amesisitiza kuwa Kilimo kina uwezo mkubwa wa kulikomboa Taifa letu kiuchumi.

“Ni lazima tuwekeze kwa vitendo katika maeneo muhimu kama Umwagiliaji, Ardhi, Masoko na Uwekezaji wa Wakulima.

Jimbo la Malinyi linaweza kuwa mfano wa mafanikio ya Sekta ya Kilimo ikiwa changamoto nilizozitaja zitapatiwa ufumbuzi wa haraka. Hivyo basi niiombe Serikali yetu kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho lao.

Napenda kumpongeza Kiongozi wetu na jemedari wetu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuikuza Sekta ya kilimo kama uti wa mgongo wa Taifa”,amesema Dk. Mecktridis.

Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yatatimia kikamilifu ikiwa Serikali itatatua kero za masoko na miundombinu katika majimbo yenye tija kubwa kama Malinyi.

Ameunga mkono hoja ya bajeti hiyo huku akitarajia utekelezaji wa haraka wa ushauri alioutoa kwa maslahi ya taifa.

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. start making over $600 a day from yodtimeshare home. I made $18,781 from this job in my spare time after college. *a11 easy wdork and his sdteady income is amazing. No skills are required for this job. All you need to know is how to copy and padste items online. Sign up today by following the details on this page.

    Here is I started.….w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    HERE——————————————⊃⫸w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  3. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

  4. Her değişim sürecinde nedense hep teknik detaylara boğuluyoruz. Bizim ysgrup projelerinde edindiğimiz en büyük tecrübe, insan faktörünü ilk sıraya koymadığınızda o planların kağıt üstünde kalması oldu. [tmbhskizmbtrezpmwc]

  5. The packaging is what is crucial here. This is the first time that photo-to-video generation has been embedded into a mainstream app like Google Photos, which the company claims has more than a billion users. Deep Nostalgia AI is intended for nostalgic use, allowing users to bring beloved ancestors back to life without including speech to prevent misuse, such as creating “deep fake” videos of living individuals. MyHeritage ensures that photos uploaded without completing the signup process are automatically deleted to protect user privacy. The animated videos are hosted on MyHeritage servers but remain the property of the user, not MyHeritage. This guide teaches you how to create touching videos of loved ones hugging using Animate Old Photos. Learn how to select the best photos and use the right prompts to bring your cherished memories to life.
    http://freestyler.ws/user/700404/liaslotloven1980
    SketchBook was the first free animation app I tried out, and I wasn’t disappointed. As a filmmaker, I could see myself using it to create text animations or storyboards. Rive completely changed the way we’re producing our content at simpleclub. Using the State Machine we’re able to support our explanations with vivid and interactive animations that really improve the way people learn with our app. Simply upload your audio file to Filmora, and select 3D cartoon or Anime as the output video style. The AI animation video generator will automatically create multiple short 3D or 2D animated videos for you. Check the detailed steps in the video tutorial. Create a 2D animation video in just 4 steps using Animaker’s AI 2D animation software PowerDirector is a video editing software that allows users to create professional-looking videos with ease. It offers features such as multicam editing, motion tracking, and AI-powered tools to enhance video quality, making it a great choice for both novice and experienced video editors.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button