Mkinga wazindua chanjo ya Suru na Rubella
TANGA: JUMLA ya Watoto 18,353 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya sindano ya surua na rubela katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga
Akizindua zoezi hilo la utoaji wa chanjo katika Kijiji cha Gezani kilichopo kata ya Manza wilayani humo Kaimu Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Juma Hamadi amesema zoezi hilo ni sehemu ya muendelezo wa hamasa ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa walengwa.
“Naomba niwahamasishe wazazi na walezi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika vituo vyote vya afya, zahanati, na maeneo lengwa ili kuhakikisha kila mtoto anapatiwa chanjo hiyo ili kujikinga na magonjwa hayo ambayo ni hatari kwa afya zao, “amesema Hamadi.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dk Salvio Wekesi amesema ugonjwa wa Surua na Rubella husababishwa na virusi vinavyoenea kwa njia ya hewa na kuleta madhara kwa watoto ambao hawajapata chanjo na wale wasiopata kinga kamilifu hivyo jamii inaendelea kupewa msisitizo wa kuhakikisha wanawapeleka watoto kupatiwa chanjo hizo ili kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo