NBAA yatoa dawa Hospitali ya Rufaa Moro

MOROGORO: ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), imetoa msaada wa dawa za dharura pamoja na vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kwa lengo la kuwasaidia watoto wasiopungua 200 wanaopatiwa huduma hospitalini hapo.

Msaada huo umejumuisha dawa za watoto, pampers, neti, sabuni za kufulia, kifaa cha kutolea maji (water dispenser) pamoja na kuchangia chupa 22 za damu, hatua iliyolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa na kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wanaopatiwa matibabu hospitalini hapo.

Akiongoza zoezi la kukabidhi msaada huo mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Prof. Siasa Mzenzi, amesema taasisi hiyo imeona umuhimu wa kusaidia hospitali hiyo kutokana na uhitaji mkubwa wa vifaa muhimu, hususan dawa na mahitaji mengine ya msingi kwa wagonjwa.


Amesema msaada huo umetolewa sambamba na mafunzo kwa wahasibu yanayofanyika mkoani humo, akisisitiza kuwa wataalamu wanapaswa kutumia fursa za mikusanyiko yao kusaidia jamii, hususan wagonjwa na watoto, ili kuwasaidia kurejea katika afya njema na kupata makuzi bora.

Katika hatua nyingine, wanachama wa NBAA wanaoshiriki mafunzo hayo wamechangisha fedha zilizotumika kulipia gharama za vipimo na dawa kwa wagonjwa 25 wasiojiweza wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo, hatua iliyolenga kupunguza mzigo wa gharama kwa wagonjwa hao na familia zao.

Kwa upande wake, Dk Azael Kyando, aliyepokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, ameishukuru NBAA kwa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitolea kusaidia jamii, akieleza kuwa juhudi kama hizo huleta faraja kwa wagonjwa na kuchangia ustawi wa jamii kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button