Moldova yakabiliwa na uhaba wa gesi

MOLDOVA : UMOJA wa Ulaya umeikosoa Urusi kwa kutumia gesi kama silaha na kuzusha mgogoro mkubwa katika sekta ya nishati nchini Moldova.

Jimbo la Transnistria, linalojitenga kutoka Moldova, limekosa gesi kutoka Urusi tangu Januari Mosi, hatua inayozidi kuzidisha uhakika wa upatikanaji wa gesi.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, alieleza kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kuunga mkono Moldova katika kukabiliana na uchokozi wa Urusi.

Kallas alizungumza na Waziri Mkuu wa Moldova, Dorin Recean, na kusema kuwa Moldova inapata msaada kupitia kuunganishwa na mitandao ya nishati ya Ulaya.

Moldova, ambayo inapakana na Ukraine, inakumbwa na changamoto kubwa baada ya kushindwa kuwapatia wakazi wake gesi na maji moto tangu Mkesha wa Mwaka Mpya.

Hali hiyo ilitokana na kampuni ya nishati ya Urusi, Gazprom, kuizimia mabomba ya gesi kufuatia mzozo wa kifedha na serikali ya Moldova.

Kwa upande mwingine, makubaliano ya usafirishaji wa gesi kati ya Ukraine na Urusi yalimalizika katika siku hiyo hiyo. SOMA: Urusi yasitisha usambazaji gesi Ufaransa ikidai malipo ya Julai

Transnistria, inayotawaliwa na vikosi vinavyoiunga mkono Urusi, inatambuliwa kimataifa kama sehemu ya Moldova, licha ya kuwa na utawala wake wenyewe.

Habari Zifananazo

Back to top button