Monalisa: Safari yangu Korea imekuwa ya ajabu

DA ES SALAAM – MWIGIZAJI wa Tanzania, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ amesema safari yake Korea Kusini kwenda kujifunza masuala ya fi lamu ilikuwa ya ajabu na kushukuru serikali kwa kupata nafasi hiyo.

Monalisa alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliosafiri na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea wiki iliyopita ambapo walijifunza namna wenzao wanavyofanya katika filamu kwa lengo la kuboresha kazi zao kuendana kimataifa.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram, Monalisa ambaye ametolewa kwenye gazeti la Korea maarufu Korean Times aliweka ujumbe wa kushukuru kwa safari hiyo.

SOMA: Nahodha Taifa Stars amsifu Samia

“Nimeheshimiwa kuoneshwa kwenye gazeti la Korean Times! Safari yangu ya hivi majuzi nchini Korea imekuwa ya ajabu, nikishiriki katika kujenga uwezo kwa tasnia ya filamu na michezo ya jukwaani.

“Tunatarajia ushirikiano wa siku zijazo kati ya tasnia ya filamu ya Korea na Tanzania. Asante kwa fursa hii na kufurahia kitakachokuja!” alisema.

Wasanii wengine walioonekana ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jackline Wolper.

Habari Zifananazo

Back to top button