Mpango ahimiza Watanzania kufuata mema ya Baba wa Taifa

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amewasihi Watanzania kuendelea kumuombea Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili aendelee kupumzika kwa amani na awe mmoja wa Watakatifu.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati alipoungana na Viongozi, Waumini pamoja na Wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika leo Oktoba 14, 2025  katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya.

Amesema ni vema kila mmoja wetu hususani viongozi kufuata mfano mwema wa Baba wa Taifa ambaye alikuwa mwaminifu kwa Taifa la Tanzania na kulitakia mema wakati wote.

SOMA: Taasisi yamkumbuka Mwalimu Nyerere

Aidha kwa niaba ya Serikali, Makamu wa Rais amewashukuru waumini na wananchi wa Mkoa wa Mbeya kwa kujitokeza kumuombea Baba wa Taifa wakati wa kumbukizi ya miaka 26 tangu kifo chake.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye katika mahubiri yake amesema Baba wa Taifa alikuwa ni mtu aliyefuata maadili mema ikiwemo mwenendo wa haki, huruma, unyenyekevu na uaminifu.

Amesema Mwalimu Nyerere aliacha urithi wa kisiasa tangu wakati wa kuhangaikia uhuru, aliacha urithi wa Muungano wa Taifa pamoja na mageuzi ya kidemokrasia.

Pia amesema kupitia Azimio la Arusha mwaka 1967 Mwalimu Nyerere aliacha urithi wa kijamii na kiuchumi ili kujenga jamii yenye usawa.

Askofu Mkuu Nyaisonga ameongeza kwamba, Mwalimu Nyerere alisisitiza elimu kwa lengo la kuondoa ujinga na kuweza kujitegemea, aliacha urithi wa utamaduni hususani kwa kusisitiza matumizi ya lugha ya Kiswahili, maadili na utu na aliweka maslahi ya Taifa mbele.

Pia amesema Baba wa Taifa alitoa mchango wa ukombozi wa kikanda na kimataifa kupitia usaidizi wake katika kuhakikisha mataifa mengine yanakuwa huru.

Alitoa mchango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushiriki kujenga diplomasia ya kusini mwa Dunia na kupigania usawa wa kiuchumi kati ya mataifa matajiri na mataifa yanayoendelea.

Amesema kupitia jitihada hizo na nyingine nyingi, ni hamasa kwa Watanzania kuendelea kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili aweze kusamehewa makosa yake na kuwa Mwenyeheri.

Ibada hiyo pia imehudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button