MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango ameyataka mabunge barani Afrika kuwekeza nguvu zaidi katika kuimarisha uwekezaji wa umma kwenye sekta ya kilimo ili kutafuta suluhu ya matatizo ya vijana pamoja na kushirikiana na serikali zao kubuni na kufadhili bunifu mbalimbali za vijana ili kuondokana na tatizo kubwa la ajira.
Dk Mpango ameyasema hayo leo jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 53 wa Mabunge Wanachama wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA -AFRICA).
Amesema ni muhimu wabunge kukuza sera na programu zinazounga mkono ajira, ufadhili wa kibunifu, kutetea maboresho ya sekta ya elimu na mafunzo pamoja na matumizi ya teknolojia kwenye sekta mbalimbali kama sehemu ya kuondokana na tatizo la ajra kwa vijana wa varani Afrika.
SOMA: Dk Mpango: Vyuo vya kilimo vishirikishwe BBT
Naye Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dk,Tulia Ackson amesema mkutano huo unaangizia masuala ya usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo changamoto ya ajira kwa vijana.
Amesema katika masuala ya chakula wabunge kupitika Chama Cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA AFRIKA) kila nchi inatoa mtazamo wake katika usalama wa chakula lakini upande Tanzania ipo tayari kuwaonesha jinsi wanavyopambana katika suala la kilimo ingawa kwa nchi za Afrika bado zinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa chakula.