Mpango elimu kwa umma waiva

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano Na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mpango mkakati wa kutoa elimu kwa umma wa miaka mitano (2022/23- 2026/27).

Akizungumza jijini Dodoma mapema leo, Mei 19,2023 bungeni waziri huyo amesema lengo la mpango mkakati huo ni kuhamasisha umma wa Tanzania kuhusu maendeleo endelevu pamoja na uhifadhi wa mazingira.

Khamis ametoa kauli wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuwapa elimu ya utunzaji mazingira wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika vyanzo na njia za mito ili wafanye kilimo bila kuleta athari za mazingira.

Advertisement

Akifafanua naibu waziri amesema mkakati huo wa elimu umehusisha namna ya utoaji elimu kuhusu matumizi ya ardhi ndani ya Mita 60 katika maeneo ya vyanzo vya maji.

“Licha ya serikali kuruhusu wananchi kufanya shughuli za kilimo kwa umbali wa mita 60 katika maeneo ya vyanzo vya maji, bado kuna changamoto nyingi za uharibifu mkubwa wa mazingira,” amesema.

Aidha, ametoa wito viongozi wa siasa kutumia uwezo wao wa ushawishi kuhamasisha jamii zinazofanya shughuli za kiuchumi katika maeneo ya vyanzo vya maji kuhifadhi mazingira