Mpiga piano Roberta Flack afariki dunia

MSHINDI wa tuzo za Grammy na mpiga piano maarufu, Roberta Flack amefariki dunia leo Februari 24, 2025 akiwa na umri wa miaka 88.

Flack alikuwa na mtindo wa sauti na muziki wa kipekee, ambao ulimfanya kuwa mmoja wa wasanii maarufu wa miaka ya 1970 na mtumbuizaji mwenye ushawishi mkubwa.

Roberta Flack Has ALS, Not Able to Sing, Rep Says

Taarifa kutoka vyombo vya habari mbalimbali vinaeleza kuwa Flack amefariki akiwa nyumbani kwake akiwa na familia yake.

Mwaka 2022, Flack alitangaza kuwa alikuwa na ugonjwa wa Lou Gehrig, na kwamba hakuwa na uwezo wa kuimba tena kutokana na ugonjwa huo.

Roberta Flack diagnosed with ALS 'making it impossible to sing' | Ents & Arts News | Sky News

Flack alijulikana kabla ya kufika umri wa miaka 30, lakini alikuwa maarufu baada ya Clint Eastwood kutumia wimbo wake maarufu “The First Time I Ever Saw Your Face” kama sauti ya mandhari kwa scene ya mapenzi maarufu katika filamu yake ya mwa 1971 “Play Misty for Me,” akiwa na mwigizaji Donna Mills.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button