Mradi wa bil 985/- elimu ya juu kupaisha uchumi

WAFANYABIASHARA wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), watanufaika na usafirishaji wa haraka wa bidhaa zao kwa gharama nafuu kwenda nchini India, baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya biashara kati ya jumuiya hiyo na serikali ya India.

Mpango huo wa pamoja wa utekelezaji utafungua fursa za biashara kati ya pande hizo mbili.

Mpango huo utazinufaisha kampuni zilizo chini ya mpango wa kiuchumi unaoendeshwa na nchi washirika wa EAC chini ya uratibu wa Sekretarieti ya jumuiya hiyo tangu 2008.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya India, Mwenyekiti Bodi ya Kodi na Forodha India  (CBIC), Ajit Kumar alisema mpango huo utakaoendeshwa kidijitali na mashirika halali ya biashara utahakikisha usalama katika mlolongo mzima wa biashara katika mipaka.

Kwa sasa MRA inawezesha wafanyabiashara wa EAC chini ya mpango wa AEO wakiwa India na pamoja na wenzao wa India katika masuala ya usafirishaji wa haraka wa bidhaa zao na kupunguza gharama na muda.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara EAC, Kenneth Bagamuhunda alisema mpango huo ukikamilishwa na kutekelezwa, utakuwa na manufaa makubwa katika kufanya biashara kati ya Afrika Mashariki na India.