Mradi wa OCP School Lab wanoga Zanzibar

ZANZIBAR; MPANGO maalumu ya upimaji afya ya udongo umezindulizwa Zanzibar ukiwa chini ya Programu ya OCP School Lab (OSL).
Uzinduzi huo umepambwa na kauli mbiu isemayo: “Napima afya ya udongo wangu kwa matumizi sahihi ya mbolea kulingana na zao.”
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili, na Mifugo, Shamata Shaame Khamis, akizungumza kwenye uzinduzi huo amesisiitiza umuhimu wa programu hiyo katika kubadilisha mbinu za kilimo Zanzibar.
“Leo, tunachukua hatua kubwa kuelekea kilimo endelevu. Kwa kuwawezesha wakulima
wetu na kuwapa zana za kuelewa udongo wao, hatuimarishi tu mavuno yao, bali
tunaboresha maisha yao na kujihakikishia usalama wa chakula kwa jamii zetu,” amesema.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau muhimu, ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa serikali,
wataalamu wa kilimo, na wakulima wa eneo hilo walio na hamu ya kujifunza kuhusu faida za
programu ya OSL.
Mpango huu unalenga kutoa uchambuzi wa udongo na mapendekezo ya
mbolea yaliyoandaliwa maalumu, kuwezesha wakulima kuboresha mavuno yao na kuongeza
tija.
“Tukishirikiana na OCP Afrika, tumejizatiti kukuza utamaduni wa ubunifu katika kilimo unaoheshimu mazingira yetu na kujenga uchumi wetu,” amesema.
Naye Ibrahim Mitawi, Mkurugenzi Mtendaji wa Showtime Zanzibar, kampuni ya usimamizi wa matukio Tanzania, pia alieleza furaha yake kuhusu mradi huo.
“Mpango huu ni mabadiliko makubwa kwa wakulima wetu. Kwa maabara za simu zinazokuja na kupima udongo moja kwa moja kwenye mashamba yao, tutawezesha wakulima kuwa na mbinu bora za kilimo na zikatumiwa na kila mtu,” Mitawi amesisitiza.
Programu ya OCP School Lab inatarajiwa kushirikiana na washirika wa ndani, ikiwa ni
pamoja na idara za kilimo za serikali, ili kuongeza upeo na ufanisi wake. Kwa kutoa mafunzo
ya mbinu bora za kilimo pamoja, mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima kufanya
maamuzi sahihi yatakayowaongezea uzalishaji na kipato.