Mwinyi atangaza mkakati mpya sekta ya afya

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inatarajia kujenga hospitali mbili kubwa za rufaa zitakazotoa huduma za kibingwa kwa maradhi ya moyo, saratani, ubongo na uti wa mgongo.

Akizungumza Ikulu Zanzibar jana, wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kati ya SMZ na Kampuni ya Jiangxi International Economic and Technical Cooperation Co. Limited, Dk. Mwinyi alisema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini.

Katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mngereza Miraji Mzee, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar, huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Jiangxi International, Bw. Peng Chao, akisaini kwa niaba ya kampuni hiyo.

Dk. Mwinyi alisema tukio hilo linaashiria dhamira ya serikali kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana nchini, akisisitiza kuwa Hospitali ya Mnazi Mmoja itabadilishwa na kuwa hospitali ya kisasa yenye miundombinu na vifaa vya kisasa vya tiba.

Amesema sekta ya afya ina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwa kuwa wananchi wenye afya bora ndio msingi wa uchumi imara na ustawi wa jamii. SOMA: ACT Wazalendo: Afya bure 100% ikishinda

Rais Mwinyi alieleza kuwa baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa hospitali katika ngazi ya msingi, wilaya na mkoa, hatua inayofuata ni kujenga hospitali tano za rufaa – moja katika kila mkoa – zitakazotoa huduma za kisasa zenye viwango vya kimataifa.

Alizitaja hospitali mbili zitakazoongezwa kujengwa ni  hospitali ya Matibabu ya Magonjwa ya Saratani, Moyo na Mifupa, na Hospitali ya Rufaa na Kufundishia Watendaji wa Sekta ya Afya, itakayojengwa Binguni.

Dk. Mwinyi alisema kukamilika kwa hospitali hizo kutawezesha Zanzibar kuachana na utaratibu wa kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, kwani huduma za matibabu ya kibingwa zitapatikana nchini kwa ubora unaokubalika kimataifa.

Akizungumzia mradi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Rais Mwinyi alisema sekta ya afya inaandika historia mpya na akaipongeza Wizara ya Afya pamoja na watendaji wote waliofanikisha kukamilika kwa mkataba wa mradi huo. Aidha, aliagiza Wizara ya Afya kusimamia kwa karibu kampuni ya ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokubaliwa.

Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja unatekelezwa chini ya ufadhili wa Benki ya BADEA, Kuwait Fund na Saudi Fund, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2027.

Habari Zifananazo

11 Comments

  1. 空调低低响着,房间冷热刚好,人却还是觉得哪里不对。有句话卡在喉咙里一整天了,现在房间这么静,它更响。你隐约看见一条缝,缝后面不一定热闹,但可能是真的。把期待放低,把感觉放真,人反而更容易碰到对的节奏。那种“再停一下”的本能出现时,往往就是转折要来了。这种说不清的劲,后来在《食神·百厨大战》里对上了。让节奏继续,比立刻下结论更重要。如果它让你不想立刻把页面划走,这就已经值了。你把这份刚刚对上的感觉护住,准备往更里走。你忽然想起白天某个没说完的瞬间,夜里它又长出了刺。你不想被推着跑,只想被带着沉,沉到一个能喘气的地方。接下来若是硬邦邦地介绍,人会退;若是顺着感觉走,人会进。你把防备再松一寸,让尚未露面的东西有机会靠近。与其把夜晚交给惯性,不如交给一个还可能让你意外的方向。把“介绍”留到你真的想知道的时候,现在先被带着。你把今天所有“应该”都暂时搁下,先听从那点隐隐的吸引。你把这份夜里的空白留着,像留一个座位,等合适的东西坐下。那种轻微的紧张并不讨厌,它让人重新变得清醒。夜还没过完,你却已经隐约知道,自己需要被带进另一段节奏里。若这点对味还在,可以从食神·百厨大战:围绕「食神百厨大战」把人物处境和选择慢慢摊开的故事往下走。

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button