MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo kuchunguza mradi wa maji wa Sh bilioni 1 uliotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) katika vitongoji saba vya kata ya Vumari.
DC Kasilda ametoa maagizo hayo alipokwenda kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ikiwemo miradi ya maji, ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Mbono unaotekelezwa na mradi wa boost utakaogharimu Sh milioni 181.
“Rais Samia Suluhu Hassani amejitahidi kutoa fedha nyingi sana kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo hii ya maji ambayo ametoa Sh 1bilioni kwa ajili ya ukamilishwaji katika vitongoji hivi saba lakini kwenye usimamizi wa miradi hii kuna changamoto, na Wananchi wanashindwa kunufaika na miradi,”
“Takukuru naomba mfuatilie haraka iwezekanavyo kuchunguza hili tujue ni kitu gani kinachofanya wananchi hawa wa vitongoji vitano kati ya saba wasinufahike na miradi ya maji na kwanini maji hayawafikii wananchi hao.”