Mradi wa umeme Mbagala wafikia 70%

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange amesema wananchi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake sasa wanatarajia kupata umeme wa uhakika kufuatia kuongezwa kwa uwezo wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala kutoka Megawati 45 za awali hadi kufikia Megawati 165.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 14,2025 mara baada ya kutembelea kituo hicho,Twange amesema ongezeko hilo ni mara mbili ya uwezo wa awali, jambo linalosaidia kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

“Kituo hiki kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali na hadi sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 70. Wananchi wa Mbagala na viunga vyake sasa wategemee umeme wa uhakika,” amesisitiza  Twange.

Aidha, Twange amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa Dola milioni 6.4 ili kufanikisha mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, amepongeza jitihada za TANESCO na kueleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kwani utamaliza kero ya umeme katika maeneo mengi ya Mbagala, Temeke, na Mkuranga.

“Kwa namna ya pekee tunaishukuru sana TANESCO kwa mradi huu kwani awamu ya kwanza ilipangwa kuanza majaribio mwezi juni mwaka huu, lakini mradi umeonyesha mafanikio mapema kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa ni viongozi,”amesema Mapunda

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button