Mshangama akabidhi mabati ujenzi nyumba ya katibu

MJUMBE wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Viti Vitatu Bara, Shamira Mshangama amekabidhi mabati kwa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa umoja huo Mwanza.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Seth Masalu, Mjumbe wa Baraza, Xavier Sanga na Katibu Ibrahim Kandumila

Advertisement

Akiwa katika ziara mkoani Mwanza, Shamira Mshangama alitembelea kuona ujenzi wa nyumba ya mtendaji wa Jumuiya ya vijana na kusisitiza kuwa pamoja na kazi zote wanazofanya ila viongozi wana jukumu la kuzingatia ujenzi wa chama hicho na Jumuiya zake.

“Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itapunguza baadhi ya gharama ambazo jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi mtendaji wetu wa vijana wa Mwanza, pia sasa itakuwa ni rahisi kwa jumuiya kujua ni wapi tunaweza kumpata mtendaji wetu kwa haraka zaidi,” ameongeza Mshangama.

Mwisho, alipata nafasi ya kuona miradi ya kiuchumi mbalimbali inayoendeshwa na UVCCM Mkoa wa Mwanza. Aliwapongeza kwa ubunifu mkubwa kwenye kuendesha miradi hio pamoja na kushirikiana vizuri na wawekezaji.