MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa Viti Vitatu Bara, Shamira Mshangama ametembelea eneo la Kisoko lenye mradi mkubwa wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.
Mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa program Maalum ya fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la ECF.
Lengo la ziara hiyo ni kuzungumza na wafugaji, kusikiliza na kutatua kero zao ambapo Shamira Mshangama ameahidi kuzitatua. Aidha amehimiza kujiandikisha katika daftari la mkazi.
Shamira katika ziara hio amekabidhi jaketi za kuokoa maisha 30 kwa wafugaji hao ili kuwahakikishia usalama wawapo kwenye majukumu yao.
Programu hiyo ilizinduliwa Januari 30, 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan, katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.