Mshikaji aliyeshauri karakana Mwendokasi Jangwani akaangwa

DAR ES SALAAM; WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema aliyeshauri karakana ya mabasi ya mwendokasi ijengwe eneo la Jangwani, Dar es Salaam awaombe radhi Watanzania kwani amewakosea sana.

Mchengera ameyasema hayo katika ziara yake kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na kudai kuwa karakana hiyo imejengwa haikuzingatia baadhi ya sheria za Baraza la Mazingira (NEMC) kwa kuwa eneo hilo kihalisia ni mkondo wa maji.

“Kwa kweli aliyeshauri karakana ya mwendokasi ijengwe pale Jangwani amewakosea sana Watanzania, eneo lile halifai na limeiletea serikali hasara kubwa, fedha nyingi zimetumika kujenga pale na sasa hivi inabidi karakana ihamishwe na pale pabomolewe, hasara sana,”amesema na kuongeza:

“Mfano sasa hivi mnataka kuhamisha Depo kwenda sehemu nyingine mnapoweka mipango yenu mjue eneo hilo lipo salama kusiwe na changamoto kama Jangwani,”amesema Mchengerwa.

Eneo la Jangwani ilipo Karakana ya Mwendokasi imekuwa ikipigiwa kelele muda mrefu na wadau wa mazingira kuwa ujenzi wake haukuzingiatia tathmini iliyofanywa na NEMC wala haukuzingatia sheria za mazingira.

Baadhi ya sheria zinazotajwa kukiukwa katika ujenzi wa karakana hiyo ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 kifungu cha Kifungu cha 57 (1). Kifungu hicho kinakataza shughuli za binadamu katika maeneo oevu.

“Kwa kuzingatia kifungu cha (2), ndani ya mita 60 hakutafanyika shughuli yoyote ya binadamu ya kudumu au ambayo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi wa mazingira au utunzaji wa bahari au kingo za mto, bwawa, au miambao ya asili ya ziwa,” ameeleza sheria hiyo.

Hata hivyo kifungu cha (2) kinampa mamlaka waziri anayehusika na mazingira kuweka miongozo ya kuendesha shughuli za binadamu ndani ya maeneo yaliyoelezwa kwa mujibu wa kifungu cha 1.

Pia uwepo wa karakana hiyo unakinzana na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya 2007, kifungu cha 25 na Sheria ya Ardhi Na.5 ya 1999 kifungu cha 7 (a-d), ambazo zinataka maeneo oevu yalindwe.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Susanames
Susanames
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Susanames
Royal
1 month ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home 16580-47065/ Doller week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………>>  http://Www.SmartCash1.com

Last edited 1 month ago by Royal
Marry
Marry
1 month ago

●Im making over $13k a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life.(ks)last month her pay check was $12712 just working on the laptop for a few hours. This is what I do, ↓↓↓↓VISIT THIS WEBSITE↓↓↓↓
HERE☛…..☛ http://Www.Smartcareer1.com

Julia
Julia
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month I have earned and received $18,539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money online.
.
.
Detail Here—————————————————————->>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x