MSLAC watoa elimu ukatili kwa wanafunzi Missenyi

ZAIDI wa wanafunzi 700 wa Shule ya Sekondari Mtukula wamepewa elimu ya  kuwasilisha  na kuripoti matukio ya ukatili katika madawati mbalimbali  wilayani Missenyi huku wakiahidiwa ulinzi wa watakapotoa taarifa.

Timu ya uratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia  wilayani humo imefika shuleni hapo kama sehemu ya kutoa elimu ya kisheria juu ya maswala ya ukatili kwa watoto  ambapo wanafunzi wengi ni waathirika wakubwa wa matukio ya ubakaji na ulawiti  pamoja na mimba za utotoni

Ofisa wa Dawati la Jinsia Kitengo cha Polisi Kyaka wilayani Missenyi, Grace Matofali ametoa wito kwa wanafunzi wanakabiliwa na matukio ya ukatili kutokaa kimya badala yake wafike katika madawati yaliyoandaliwa Kwa ajili ya Kupata ufumbuzi.

Amesema kuwa hakuna siri itakayofika kwa mtu yeyote au kumutaja mwathirika wa tukio la ubakaji wa ulawiti pale atakapokuwa ametoa taarifa .

“Najua mnapokea vitisho vingi vya kahawa na watu wanaowafanyia ukatili anasema ukisema nitakuua ,hakuna atakaye kuua njoo unipe taarifa  serikali itakulinda  kwa nguvu zote msikubari kutumika  njooni mtoe taarifa mama Samia yuko kwa ajili yenu,”amesema Matofali.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtukula  wametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule na kuteua shule yao kufikiwa na elimu juu ya maswala ya kisheria yanayohusu ukatili kwani wanafunzi wengi wanakabiriwa na vitisho kutoka kwa waharifu wenye Nia ovu ya kutenda makosa ya ukatili kwa watoto.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button