Msonde afundisha wanafunzi, kupima KPI

TABORA: NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde ameingia darasa na kuwafundisha somo la Hisabati wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Ulaya iliyopo katika halmashauri ya wilaya Igunga Mkoani Tabora.
Msonde amefundisha somo hilo leo Agosti 29, 2023, baada ya kufanya ziara katika shule hiyo na kukagua hali ya utoaji wa elimu mashuleni na kukagua utekeleza wa vigezo vya kuboresha elimu nchini (KPI).
Aidha, Dkt. Msonde alitaka kujihakikishia utayari wa wanafunzi hao wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtiani wa kuhutimu elimu ya msingi mwezi Septemba 2023.



