‘Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu’

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima wanaotumia maji ya Mto Ruvu kwa shughuli za kilimo kusitisha matumizi hayo kwa muda hadi pale mvua zitakapoanza kunyesha kwa wingi ili kutoathiri shughuli za uzalishaji na usambazaji wa maji kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.
Kunenge ametoa wito huo wakati alipofanya ziara katika mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu kwa lengo la kukagua Hali ya uzalishaji maji na upatikanaji wa maji katika chanzo cha Mto Ruvu.

“Mabadiliko ya hali ya hewa hususani kuongezeka kwa joto yamesababisha kupungua kwa kiwango cha maji, hususan katika eneo la Ruvu Chini, hali hii pia imesababishwa na shughuli za kilimo zisizo rasmi kando kando ya mto kwa watu kulima bila vibali,” ameeleza Kunenge.
SOMA: Watumiaji mto Ruvu wawekwa hadharani
Kunenge ameongeza kuwa uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Chini umepungua, japokuwa si kwa kiwango kikubwa, huku Ruvu Juu ikiendelea kuwa na kiwango cha maji cha kuridhisha.

“Nitoe wito kwa watumiaji wa maji, hususani wanaofanya Kilimo kusitisha matumizi hayo kwa muda mpaka pale mvua zitakapoanza tena na maji kuongezeka mtoni, kwasasa maji haya yabaki kwa matumizi ya binadamu tu, lakini pia tutafuatilia wale wanaofanya kilimo kwa kutumia maji ya mto huu bila vibali na kusababisha changamoto katika mto,” amesema.
Vile vile Kunenge amesema, kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upungufu wa maji, kwani bwawa hilo litaruhusu uhifadhi wa maji ya kutosha bila kutegemea mvua za msimu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameitaka Bodi ya Bonde la Maji Wami-Ruvu (WRBWB) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kufanya jitihada za haraka na upesi kuboresha maeneo yenye changamoto katika Mto Ruvu yanayosababisha maji kupotea na kupunguza wingi wa maji mtoni ili wananchi waendelee kupata huduma ya maji yenye uhakika.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com