Mtunza bustani jela maisha kwa kumnajisi darasa la kwanza

SHINYANGA; Kahama. MAHAKAMA  ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, imemuhukumu mkazi wa Kijiji Cha Chapulwa, Kata  ya Mwendakulima, Kaliyango Maganga (55)  kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka nane 8) anayesoma darasa la kwanza.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,  Christina  Chovenye ametoa hukumu baada ya kuridhika kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo kwa mtoto huyo mara kwa mara,ambapo alifikishwa mahakamani Julai 30, 2023.

Hakimu Chovenye alisema mshtakiwa  alikuwa na kazi ya umwagiliaji  bustani ya maua nyumba ya jirani na mtoto huyo, ambapo alikuwa akimvizia wakati akienda shule walezi wake wakimuacha peke yake na kwenda  kwenye shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa  Mwime.

“Walezi wake ambao ni babu na Bibi walikuwa wakiondoka na kumuacha ndipo mtuhumiwa alikuwa akimchukua na kumnajisi, huku akimueleza asimwambie mtu akisema atamuua,”amesema Chovenye.

Hakimu  Chovenye amesema  mtoto mwenyewe alisikilizwa na kutoa maelezo ya kunajisiwa na mtuhumiwa mara kwa mara na  vipimo vya daktari  vimethibitidha,  hivyo mahakama  haikuwa na shaka lolote juu ya utoaji wa hukumu hiyo.

Pia ushahidi wa walimu ambao waligundua mtotp huyo kunajisiwa na kueleza kuwa kila siku alikuwa akichelewa shule na akifika anakuwa amechoka na mwenye maumivu makali.

Mshtakiwa  akijitetea aliomba apunguziwe adhabu hiyo kwa madai ni mzee na anategemewa na familia.

 

 

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button