Mwalimu jela miaka 14 ubadhirifu fedha za madawati

MANYONI, SINGIDA: John Mtaki, Mwalimu wa Sekondari ya Kintinku Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya mahakama kumkuta na hatia ubadhirifu wa Sh milioni 3.5.

Kiasi hicho kilitolewa kwenye akaunti ya shule kabla ya mwalimu huyo kukabidhiwa kwa ajili ya kutengeneza madawati.

Kesi ya jinai namba 14545/2026 ilifunguliwa Juni 26, 2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Manyoni dhidi Mwalimu huyo.

Mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu na ufujaji kinyume na kifungu cha 28 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2023, Wizi kwa mtumishi wa Umma kinyume na kifungu cha 270 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2023.

SOMA: TAKUKURU yatumia ngoma za asili vita dhidi ya rushwa 

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia ana Kupambana na Rushwa (TAKUKURU, Wilson Ntiro alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, George Kapama, kuwa mnamo Julai 20, 2024 mshtakiwa huyo alilipwa  kiasi cha 3,500,000 taslim kutoka akaunti ya shule ya sekondari Kintinku kwa ajili ya kutengeneza madawati ya madarasa mawili.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka alidai, Mwalimu huyo hakutekeleza jukumu hilo alipofunguliwa mashtaka hayo.

Kesi hii ilitolewa hukumu Oktoba 29, 2026 ambapo Mahakama imemtia hatiani kwa kifungo cha miaka 14 jela.

Aidha Hakimu Kapama aliamuru pikipiki  ya mwalimu huyop iliyokuwa inashikiliwa na TAKUKURU itaifishwe, iuzwe na fedha hizo zitumike kutengeneza madawati ya shule.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button