Mtwara wahamasishwa mapokezi ya Mwenge

MKURUNGEZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Erica Yegella leo ameongoza kamati ya uhamasishaji  wilayani humo kutembelea kata na vijiji katika halmashauri hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Aprili 3, 2023.

Yegella pia ametembelea na kukagua miradi ambayo itapitiwa Mwenge huo, ikiwemo mradi wa shamba la mikorosho, mradi wa maji na mradi wa bweni la watoto wa kike wenye mahitaji maalumu.

Harakati hizo zinafanyika ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kuzinduliwa kwa mbio za mwenge huo kitaifa katika mkoa wa Mtwara, Aprili mosi mwaka huu.

Baada ya uzinduzi, Mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri ya Mtwara Vijijini Aprili 3-4.

Mratibu wa Mbio za Mwenge Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Nicholas Muya amesema jumla ya miradi mitano yenye thamani ya Sh bilioni 2.2 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button