Muda wakwamisha mabadiliko ya sheria kupelekwa bungeni

SERIKALI haitapeleka bungeni mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma ya Habari Namba 12 ya Mwaka 2016 ambayo ilipangwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa 10 wa Bunge la 12 unaoendelea Dodoma.

Kutokana na hatua hiyo sasa mabadiliko ya sheria hiyo itawasilishwa katika Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia Aprili mwaka huu.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Gerson Msigwa alisema Dodoma jana kuwa kutowasilisha muswada huo kumetokana na ufinyu wa nafasi katika bunge linaloendelea.

“Bunge la Januari ni mahususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za kamati za kudumu za Bunge na Serikali ilipanga kuwasilisha miswada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali ili wabunge wazifanyie marekebisho tuendelee kuzitumia,” alisema Msigwa na kuongeza:

“Niwahakikishie wadau kuwa maandalizi yote yamekamilika kilichokwamisha kwanza ni muda, kwa mujibu wa Mkutano wa 10 una vikao 10 na huwezi kuzidisha, hivyo hakukuwa na muda wa kutosha wa kuwasilisha muswada huo.”

Habari Zifananazo

Back to top button