Mufti amteua Ngeruko kuwa Naibu Kadhi Mkuu

Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi

MUFTI na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally amemteua Shehe Ally Khamisi Ngeruko kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania.

Taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa umma imeeleza kuwa pia Mufti amemteua Mhasibu Mkuu wa Bakwata, Mwenda Said Mwenda kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Utawala na Fedha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Taifa Bakwata na Msemaji wa Mufti, Shehe Khamis Mataka, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Nuhu Jabir Mruma amemteua Twahir Al-musawaa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Bakwata makao makuu.

Advertisement

Mruma pia amemteua Shehe Othman Ali Kaporo kuwa Mkurugenzi wa Kurani na mambo ya dini Bakwata makao makuu.

Mataka ameeleza kuwa pia Mruma amemteua Tabu Kawambwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uhusiano na Usalama wa Ndani Bakwata makao makuu.

Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Aprili 10, mwaka huu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *