MUHAS waja na mpango wa mazoezi usimamizi kitabibu

DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo maalum ya kitaalamu kwa wakufunzi wa mazoezi ya viungo (gym instructors) na wasimamizi wa kumbi za mazoezi (fitness managers),ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja wanaopelekwa kufanya mazoezi kwa sababu za kitabibu.

IIrene Mzokolo akifafanua namna vifaa vya ‘GYM’ vinavyofanya kazi.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa alisema mpango huo unalenga kulinganisha huduma za mazoezi ya viungo ya viwango vya kitaifa vya afya.

Prof Kamuhabwa akijaribu kuona namna gani vifaa hivyo vinafanya kazi katika eneo la kituo cha magonjwa ya moyo Mloganzila.

“Lengo letu ni kuwajengea uwezo waendeshaji wa kumbi za mazoezi ili waweze kutoa huduma kwa kufuata taratibu za kitaalamu za afya,” amesema Prof Kamuhabwa.

SOMA ZAIDI: Wananchi wajitokeza kwa wingi uchunguzi magonjwa ya moyo

Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyopo katika kituo hicho.

Profesa Kamuhabwa amesema kama sehemu ya mpango huo, MUHAS itazindua kituo kipya cha mazoezi ya viungo mapema wiki hii, ambacho kitakuwa kinatoa vyeti vya mazoezi kama ilivyo kwa dawa zinazotolewa kwa agizo la daktari.

Prof Kamuhabwa akiendelea kujaribu namna vifaa hivyo vinavyofanya kazi

Kwa upande wake, mtaalamu wa fiziolojia Irine Mngolokolo,amesema ‘gym’ hiyo mpya imeundwa mahsusi kwa ajili ya watu wenye changamoto za kiafya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button