Museveni: Tunaweza kuendelea bila kuungwa mkono
KAMPALA; RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni hana wasiwasi wowote baada ya taifa lake kuondolewa katika mpango maalumu wa kibiashara wa Marekani na Afrika (AGOA)
Rais wa Marekani Joe Biden alisema nchi nyingine tatu za Afrika zitaondolewa katika umoja huo akitaja sababu za kuondolewa huko ni ukiukuaji wa haki za binadamu unaotambulika kimataifa.
Museveni aliwakosoa vikali Marekani akisema kuwa taifa hilo linadhani nchi za kiafrika haziwezi kujiendeleza wenyewe bila misaada kutoka ughaibuni.
“Tuna wezo wa kufikia malengo yetu ya ukuaji na mabadiliko bila hata kuungwa mkono”, Museveni amesema
Katika hatua nyingine Rais huyo aliipongeza Marekani kwa kuendeleza ufadhili wa dawa za VVU na kuongeza kuwa serikali yake inajipanga kutafuta suluhisho la upatikanaji wa dawa hizo ikiwa wafadhili watajiondoa.