Mv Serengeti yapinduka, yazama Mwanza

Mwanza

MWANZA; MELI ya Mv Serengeti imepinduka na kuzama kwenye Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa imefungwa katika gati bandarini hapo.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) imesema meli hiyo imepinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma jana, saa saba usiku.

Imeeleza kuwa Tashico imeshirikiana na timu mbalim bali za wataalamu kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wadau wengine katika juhudi za uokoaji.

Advertisement

“Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini tatizo utakapokuwa umefanyika,” ilisema taarifa. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye Ziwa Victoria mwaka 2016