Mvulana ajinyonga akitoka kucheza mpira

JUMA  Hamis  (15), mkazi wa mtaa wa Iwelyangula, Kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga, amekutwa amejinyonga kwa kamba kwenye mti katika bustani ya matunda.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu Septemba 12, 2022 majira ya saa 12 jioni, ambapo kabla ya kujinyonga inadaiwa marehemu alikuwa eneo hilo na rafiki zake wakicheza mpira wa miguu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Iwelyangula, Robert Mnyeleshi, akizungumza asubuhi leo, ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa mfanyakazi wake akichunga mifugo, akitokea mkoani Kigoma na kwamba alipomaliza kucheza mpira na wenzake jana hakurudi nyumbani.

Amesema walianza kumtafuta usiku jana, bila mafanikio, hadi asubuhi hii walipokuta ananing’inia kwenye mti, eneo walilokuwa wakicheza mpira na wenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,  Janeth Magomi amethibitisha kupokea taarifa ya kifo hicho na upelelezi unafanyika, kwani hakuna ujumbe wowote ulioachwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x