Mwakioja achukuwa fomu Mkinga

TANGA: MGOMBEA ubunge jimbo la Mkinga kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM )Twaha Mwakioja amechukuwa fomu kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuomba kuteuliwa nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mwakioja amekabidhiwa fomu na Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi wa jimbo hilo leo Agosti 26 wilayani Mkinga.

SOMA ZAIDI

Inec yazidi kunoa wanahabari Uchaguzi Mkuu

Baada ya kukabidhiwa fomu Mwakioja amekishukuru chama chake chini ya Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo.

“Ikiwa tume itaniteuwa kugombea nafasi hii naahidi kufanya kampeni za kiustaarabu zenye kujali utu na hatimae kupata kura nyingi za Urais,ubunge na udiwani nina imani tutapata ushindi wa kishindo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button