Mwamnyeto: Haturingi kufuzu nusu fainali
NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika hakuwapi kiburi cha kujiona bora kuliko timu nyingine nchini
Akizungumza na HabariLEO, mchezaji huyo ameeleza kuwa siri ya mafanikio hayo ni kutokana na kuiheshimu kila timu waliyokutana nayo na kucheza kwa kufuata maelekezo, ambayo wamepewa na benchi lao la ufundi linaloongozwa na Nasreddine Nabi.
“Ukweli ni kwamba hatujioni bora kwa kuwa tumefika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ingawa tunastahili pongezi kwa kazi tuliyoifanya, lengo letu ni kufika fainali, lakini tukitanguliza mbele heshima kwa kila timu ndani na nje ya Tanzania,” amesema Mwamnyeto.