‘MWANA FA’ mgeni rasmi Simba, Vipers

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MWANA FA’ anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba SC na Vipers utakaopigwa Jumanne Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo na kuongeza kuwa wapinzani wao Vipers watawasili nchini Jumatatu kwa ajili ya mchezo huo.

Ahmed Ally amesema mchezo huo utakuwa wa kuamua hatma ya timu hiyo, hivyo wamejipanga kuhakikisha wanashinda ili kuwapa matumani mazuri ya robo fainali.

“Tulikwenda kufufukia Uganda, na kweli tumefufuka. Jumanne ni mechi ya marudio katika mechi hii tunakwenda kuamua hatma ya Simba kwenye michuano ya CAF. Tukimpiga tutafikisha alama 6 na kuanza kuchungulia robo fainali”. Ahmed Ally.

Amesema tiketi zimeanza kuuzwa, Sh. 3,000 – Mzunguko, Sh. 10,000 – VIP C, Sh. 20,000 – VIP B, Sh. 30,000 – VIP A, Sh. 150,000 – Platinum lakini kuna Simba Executive Tickets kwa ajili ya wateja wetu walio maofisini”. Ahmed Ally.

Habari Zifananazo

Back to top button