NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema anataka kuvunja rekodi ya kuishia hatua ya makundi katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mwana FA alisema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika Moshi, Kilimanjaro.
Alisema serikali ina majukumu mawili katika kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika moja ni kuandaa miundombinu na pili ni kuandaa timu na kuongeza itakuwa ajabu endapo timu ya Taifa itaondolewa mapema.
“Nataka kuvunja rekodi ya kuishia makundi na mimi napenda sifa hivyo hii sifa naitaka,” alisema Mwana FA.
Alisema baada ya kuandaa mashindano ya Mataifa ya Afrika ya Chan na Afcon wanataka Tanzania ifuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2030 na Tanzania kuwa taifa kubwa kisoka Afrika.
Kadhalika alipongeza uongozi wa TFF kwa maendeleo makubwa katika soka yaliyopatikana katika kipindi kifupi na kusema serikali haitakuwa kikwazo kufanikisha timu yeyote inayowakilisha nchi kimataifa.
Aidha alisema ana imani kubwa kuwa Simba na Yanga zitafuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya kimataifa.
Yanga inashirikia Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba wao ikishiriki Kombe la Shirikisho la Afrika.
“ Serikali tuko nyuma ya timu hizo kuhakikisha zinafanya vyema na kupeperusha bendera ya nchi na zitafuzu kucheza robo fainali,” alisema Mwana FA.
Mwana FA ametoa wito wa wadau wa soka nchini kujitokeza na kushirikiana vyema na TFF ili nchi iweze kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.
a mwenyeji pamoja na Kenya na Uganda ambayo yanatarajiwa kuanza Februari Mosi hadi 28 mwakani.
Akizungunza katika Mkutano Mkuu wa kawaida wa 19 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Morocco alisema timu yake itaanza maandalizi mapema ili kufanikisha hilo.
Alisema kuwa anajua ana wachezaji wengi vijana ambao wanafanya vizuri katika ligi zao hivyo ana imani kubwa kuwa watapambana na kushinda katika kila mchezo wataocheza.
Morocco alisema itakuwa ni heshima kubwa kwao kama wenyeji kuchukua ubingwa na hilo linawezekana endapo wataweka juhudi lakini pia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wa soka.
“Najua siyo rahisi kwani timu zote ambazo zinashiriki zipo vizuri lakini nina imani kubwa na timu yangu kwani tunalitaka kombe na uwezo tunao na wachezaji wazuri pia tunao,” alisema Morocco.
Alisema ataita kikosi chake mapema ili kufanya maandalizi mapema na kurekebisha upungufu uliojitokeza katika michezo waliyocheza ili kufanya vyema katika mashindano hayo.
Morocco alisema mashabiki na wapenzi wa soka nchini wasiwe na wasiwasi kwani ataita kikosi bora chenye ushindani mkubwa.