Mwanariadha Jeshi la Polisi avunja rekodi Uingereza

MWANARIADHA wa Jeshi la Polisi Konstebo Transfora Mussa ameshinda mbio za kilomita 10 za Fulham zilizofanyika Uingereza huku akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa kukimbia muda mfupi zaidi.

Mwanariadha huyo ambaye amepata medali ya dhahabu, amevunja rekodi hiyo kwa kutumia dakika 31:53 tofauti na rekodi ya iliyowekwa 2023 na mwanariadha kutoka Kenya aliyeshinda kwa kutumia dakika 33:11 katika mashindano hayo.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya mwanariadha huyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege KIA, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Alphonce Bandya kwa niaba ya Kamanda wa Polisi pamoja na kumpongeza mwanariadha huyo kwa kuliletea sifa Jeshi hilo, amesema wataendelea kutoa ushirikiano wakati wote kwa timu hiyo ili ipate mafanikio zaidi.

SOMA: Kishindo cha Wanariadha waliofanya vizuri Japan

Kwa upande wake Konstebo Transfora amesema nidhamu pamoja maandalizi mazuri aliyoyafanya ndio msingi wa mafanikio hayo ambapo ameahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.

Kocha Msaidizi wa Timu hiyo Sajenti Oswald amesema usikivu na nidhamu wakati wa maandalizi katika kambi yao sambamba na kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa uongozi mzima wa Jeshi la Polisi pindi wanapohitaji ndio chachu ya mafanikio yao.

Habari Zifananazo

Back to top button