Mwanaume aliyefariki miaka 128 iliyopita hatimaye kuzikwa

READING, Marekani: Mwanaume mmoja aliyefariki miaka 128 iliyopita na mwili wake kusalia katika jumba la huduma ya mazishi huko Reading, Pennsylvania nchini Marekani atazikwa wiki hii, ishara ya kuhitimisha safari yake hapa duniani.

Mwanaume huyo ambaye alipachikwa jina la Stoneman Willie alifariki gerezani Novemba 19, 1895 baada ya figo kushindwa kufanya kazi kutokana na kile kilichotajwa kuwa ulevi uliokithiri. 

Kwa bahati mbaya alikaushwa na daktari aliyekuwa akijaribu njia mpya ya kuhifadhi mwili, watoa huduma ya mazishi, Auman walisema.

Willie ameonekana kwenye jeneza akiwa amevalishwa suti na tai na mkanda mwekundu kifuani. Nywele na meno yake yamebakia sawia huku sura ikichukua muonekano wa ngozi.

Willie hakuweza kutambuliwa na ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwa alitumia jina la uongo wakati alipo kamatwa. Maafisa wa eneo hilo walikata tamaa ya kutafuta jamaa zake.

Taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji huduma ya mazishi iliiomba serikali iwaruhusu kuuhifadhi mwili huo badala ya kuuzika ili kupata matokeo ya jaribio la daktari kuhusu uhifadhi wa maiti.

Auman imesema baada ya miaka kadhaa imefanikiwa kumtambua Stoneman Willie kwa kutumia nyaraka za kihistoria na itataja jina lake baadaye wiki hii wakati wa mazishi.

Hadi sasa, hakuna mengi yanayojulikana juu yake zaidi ya mizizi yake ya Kiayalandi.

“Hatumrejelei kama mummy. Tunamtaja kama rafiki yetu Willie,” alisema Kyle Blankenbiller, mkurugenzi wa mazishi. “Amekuwa picha kama hii, sehemu ya hadithi sio tu ya zamani ya Reading lakini hata ya sasa.”

Kabla ya mazishi, jiji la Reading litamkumbuka mtu ambaye amekuwa sehemu ya ngano za jiji hilo kwa vizazi.

Siku ya Jumapili, wakaazi wa eneo hilo walifurika barabarani kusherehekea kumbukumbu ya miaka 275 ya Reading kwa gwaride la kupendeza lililojumuisha gari la kubeba maiti likibeba jeneza la Willie.

Wiki hii yote, Willie ataonyeshwa kwenye Nyumba ya Mazishi ya Auman. Siku ya Jumamosi, atafanya safari yake ya mwisho katika mitaa ya Reading na atazikwa kwenye makaburi ya eneo hilo, ambapo jina lake halisi litaandikwa kwenye jiwe lake la kaburi.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button