Mwanaume changia damu mara 3 kwa mwaka inaruhusiwa

KATIKA kuadhimisha siku ya kuchangia damu Duniani,Mpango wa Damu Salama, Kanda ya Mashariki umesema mwanaume anaweza kuchangia damu mara tatu kwa mwaka huku mwanamke akiwa na uwezo huo mara nne.

Ofisa Mhamasishaji  Mpango huo Kanda ya Mashariki  Fatma Mjungu amesema  hayo leo Juni 14, 2023 katika kuadhimisha siku ya damu na kuwashukuru wote waliojitokeza kuchangia huduma hiyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine.

Amesema hakuna mbadala wa damu  na kuchangia kwa ajili ya wahitaji inawezekana kufanya hivyo mara  kwa mara.

Kwa upande wake Meneja Mpango wa Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Pendael Sifuel  amesema mtambo wa apheresis wa kuchakata damu  una uwezo wa kuchukua mazao ya damu yanayohitajika kwa mgonjwa, huku damu ikiwa mwilini mwa  mchangiaji.

Amesema mazao  ya damu yanayoweza kuchakatwa  ni pamoja na chembe nyekundu ya damu, plasma na chembe sahani.

Kuhusu mazao ya damu amesema mtambo huo waliokaboidhiwa na serikali una uwezo wa kuchakata  damu, huku damu ikiwa mwilini mwa mchangiaji na inatenganisha  mazao  hayo yad amu kulingana na kiwango kinachohitajika kwa wagonjwa.

“Mwanzoni ilikuwa lazima mchangiaji atoe damu, ambayo mhitaji huwekewa yote kama ilivyo bila kujali mazao yanayotajika katika mwili wake, lakini kwa sasa mashine hiyo imeweza kutenganisha mazao yad amu, huku damu ikiwa mwilini mwa mchangiaji,” amesema Sifuel na kuongeza kuwa mwaka huu wanazindua kadi za kielektroniki kwa wachangiaji damu.

Amesema  teknolojia ya kugawa damu kwenye mazao yake ipo kwenye hospitali  mbalimbali  nchni ikiwemo za mikoa n ahata za  rufaa.

Amesema teknolojia hiyo inasaidia badala ya kupewa damu yote halafu mwili ndio uchague kinachitajika kwa sasa, upo uwezekano wa kupewa zao la damu kulingana na uhitaji wa mgonjwa.

Kuhusu maadhimisho amesema hufanyika ili kuwaenzi wale waliochangia damu kwa wagonjwa na kuokoa maisha yao na kwa mwaka huu, walengwa watapewa vyeti vilivyosainiwa na Waziri husika kwa lengo la kuwashukuru.

Amesema kauli mbiu yam waka huu ni pamoja na Changia Damu, haswa mazao yad amu, changia mara kwa mara, ikifafanua kuwa sio kila mgonjwa anayehitaji damu huhitaji damu yote bali wapo wanaohitaji baadhi ya mazao hayo yad amu.

Sifuel amesema kila mchangiaji wad amu anapochangia lazima ichakatwe kulingana na hitaji la mgonjwa na kutolea mfano mgonjwa wa ajali huhitaji zaidi chembe nyekundu yad amu ambayo husaidia hewa ya oksijeni mwilini.

Amesema chembe sahani ya damu husaidia wagonjwa wa saratani ambao wakati mwingine hutokwa na damu bila kuganda hivyo zao hilo husaidia kugandisha damu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button