Mwenge wa Uhuru wakagua miradi ya Sh Bil 5 Iramba

SINGIDA; MWENGE wa Uhuru umekimbizwa umbali wa Km 68.1 umetembelea, umekagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 5 katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amesema miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2024 katika wilaya hiyo ni mradi wa ujenzi wa Barabara ya Old Kiomboi Km 1.5, uwekaji Jiwe la Msingi shule mpya ya Sekondari Iramba, kutembelea mradi wa ujenzi wa Chuo cha Veta.

Pia uzinduzi wa huduma katika jengo la Mama na Mtoto, jengo la kuhifadhia maiti na mitambo ya kuzalisha hewa ya oksijeni katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo Old Kiomboi, kikundi cha vijana Emirates, kuweka Jiwe la Msingi na uendelevu wa mradi wa maji Kijiji cha Makunda.

SOMA:https://habarileo.co.tz/mwenge-wa-uhuru-kukagua-miradi-ya-sh-bilioni-7-nyanyamba/

“Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Iramba umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo hakuna mradi uliokataliwa,” amesema DC Mwenda.

 

Habari Zifananazo

Back to top button