Mwenge wa Uhuru wazindua miradi ya bil 51.8 Ilala

MWENGE wa Uhuru umewasili jijini Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuanza mbio zake katika Wilaya ya Ilala, ambapo umetembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 51.8.
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema miradi hiyo inalenga kuboresha huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo sekta za afya, maji, ulinzi na usalama pamoja na miundombinu ya barabara.SOMA: Uzinduzi Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 Pemba
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amewasisitiza wananchi hususan vijana kudumisha amani, utulivu na mshikamano, akieleza kuwa Mwenge wa Uhuru unabeba ujumbe wa kuhamasisha maendeleo na umoja wa kitaifa.

Awali, akipokea Mwenge huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema kuwa katika mkoa huo Mwenge wa Uhuru utatembelea jumla ya miradi 35 yenye thamani ya shilingi bilioni 113.5.
Kwa mwaka 2026, Mwenge wa Uhuru unabeba kaulimbiu isemayo: “Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo.” Miradi iliyotembelewa Ilala ni pamoja na kitega uchumi cha DDC Kariakoo, barabara ya Lindi, kisima cha maji, Kituo cha Afya Mchikichini, Shule ya Sekondari Kitunda Relini, Kituo cha Polisi Bonyokwa na mradi wa kikundi cha vijana cha Fighters.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site
thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. de.yandaz.com
thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. usa.yandaz.com
thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. de.yandaz.com