Mwenge wapitia miradi ya bil 1.7/- Nanyamba

MTWARA: MIRADI saba ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 1.7 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara.

Katika miradi hiyo saba iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 ikiwemo miradi 2 kuzinduliwa, kuweka jiwe la msingi mradi 1, kuona na kukagua miradi 4 huku ukikimbizwa kwenye umbali wa kilomita 76.

Miongoni mwa miradi hiyo iliyopitiwa na Mwenge ikiwemo kikundi cha vijana  Manson kinachojishughulisha na ufyatuaji tofali kilichopatiwa mkopo wa asilimia 10 na halmashauri hiyo.

Miradi mingine ni uwashaji umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mradi wa uchimbaji kisima cha maji chini ya ardhi shule ya Amali Chikota, mradi wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi na salama kwa kupikia na mingine.

Akizungumza alipozindua kikundi hicho cha vijana cha ufyatuaji tofali, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda ameendelea kuwahamasisha vijana kwa ujumla kwenye halmashauri hiyo kuhamasika na kujiunga na vikundi mbalimbali vya ujasiliamali ili waweze kupata mkopo huo.

“Mikopo hii imekuwa mkombozi kwa vijana, wanawake na wenye mahitaji maalum, nitumie fursa hii kumpongeza sana Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa maelekezo kwenye halmashauri kutoa mikopo ya asilimia 10″amesema Wazo

Baadhi ya wanakikundi wa kikundi hicho cha ufyatuaji tofali akiwemo Hashimu Jabili ameishukuru halmashauri kwa kuwawezesha mkopo huo kwani sasa wanakuza kipato chao.

Aidha Mwenge wa Uhuru katika halmashauri hiyo ya mji Nanyamba umepokelewa jana katika kijiji na kata ya mnima ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini mkoani huo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. The Best opportunities To Earn $22,000/Month. We all spend a lot of time on social media every day – Facebook, Instagram, Snapchat, Twitter, and the list goes on. If you’re used to getting a lot of likes or comments, or if you’re great at motivating others through your posts, you might want to consider turning this into a profession. It appears unbelievable but you won’t forgive yourself if you do not check it….

    HERE →→→→w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button