Mwenyekiti ALAT amuombea Rais Samia

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) Taifa Murshidi Ngeze amefanya dua kumuombea Rasi Samia Suluhu kwa kuwashirikisha wadau, viongozi wadini zote na wananchi wa Mkoa wa Kagera kumshukuru Mungu baada ya kupata ajali iliyepelea kupoteza baadhi ya viungo vyake mwaka 2022.
Maelfu ya ya wananchi mkoani Kagera walikusanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Rukoma kumushukuru Mungu kwa uponyaji wa mwenyekiti huyo aliyepata ajali mwishoni mwa mwaka 2022 mkoani Pwani na kupeleka kukatwa mguu wake mmoja na kurejea katika majukumu yake karibuni.
Amesema alimaliza kutimiza majukumu yake kama kawaida mkoani Kagera na akaondoka kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kikao na ndipo alivaana na gari aina ya fuso moja kwa moja na akalazimika Kufanya njia za kuokoa maisha yake jambo ambalo limepelekea ulemavu wa kudumu.

“Kitu kikubwa ambacho sitasahau ni pale nilipoona fuso liko mbele yangu kunivaa ,Mungu alinipa ujasili wa kulikwepa lisinisage nikabiringika na kuanguka vibaya nakumbuka kijana mmoja alinifikia nikipiga kelele nikamuomba maji ya kunywa akaninyima,”
“Amesema nisijaribu kunywa akakimbia akaleta mipira ya baiskeli akanifunga miguu na badae nikapelekwa hospitali hadi nilipojitambua mpaka kukubari mabadiliko ya kukatwa mguu wangu na kubaki na mguu mmoja ambao nao umebaki kwa kupata matibabu makubwa kwani nilipaswa kukatwa yote,”amesema Ngeze.

Amesema kitu ambacho kilimpa ujasiri na nguvu ni baada ya kuzinduka akakutana na waziri wake wakati huo Angelina Kairuki, na badaaye akakutana na Makamu wa Rais Dk Philipo Mpango ambaye alitumwa na Rais Samia kujua afanye nini ili aweze kupona ambapo alisema kuwa aliwasiliana na Rais kuanzia mwanzo wa safari yake ya kuumwa mpaka anapona na kurejea katika majukumu yake.
“Nimefanya dua hii leo kwa kushirikiana na wadau na marafiki zangu wengi lakini natumia wasaha huu kuwaambia kuwa Raisi wetu anaroho nzuri sana ndio maana leo kwa kushirikiana na viongozi wa dini tunamuombea mama yetu Mungu aendelee kumpa maisha marefu na wakati huo tunaombea uchaguzi mkuu kuwa uchaguzi wa amani kwa watu wote ,nawashukuru wote kwa kuwa na mimi katika wakati wote,”amesema.

Shekhe wa Wilaya ya Bukoba, Twahili Saidi amesema anamjua Ngeze kama diwani wa miaka 10 kata Rukoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba hivyo ni mtu ambaye anayamudu majukumu na kuwa ameimarika aendelee kupewa nafasi ya kuwatumikia wananchi kwani kwa sasa yuko imara na amerejea katika majukum yake.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima pamoja na kuungana na viongozi wa dini kufanya maombi hayo aliwaondoa hofu wananchi kuwa kigezo cha Ngeze kupungukiwa na viungo vyake akiwezi kumuondoa katika michakato ya uongozi hivyo watulie na waendelee kumuombea maisha marefu ili akihitaji tena kuwatumikia apate nafasi hiyo.
“Hakuna kitu kinachoweza kumuondoa ila kupitia maelekezo ya Rais Samia ya kumthibisha kiongozi huyo mpaka akapona vizuri ni vyema wananchi nyote tulipe shukrani hizo kwa kumpigia kura kwa wingi sana, “alisema Sima.



