Mwenyekiti Bodi ya Ligi ajiuzulu

DODOMA; MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB), Steven Mnguto amejiuzulu wadhifa huo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) usiku huu, Wilfred Kidao imeeleza kuwa pia Rais wa TFF amemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa bodi hiyo, Almasi Kasongo.



