HATMA ya nani atapokea kijiti na kushika nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujulikana Novemba 30 mwaka huu jijini Arusha kwenye mkutano wa kawaida wa marais utakaofanyika jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronika Nduva alisema wakuu wa nchi watakapomaliza mkutano wao wa ndani ndipo watatokavna majibu ya nani atashika nafasi ya mweyekiti wa EAC kwa muda wa mwaka mmoja
“Wakuu wa nchi ndio wataamua nani atashika nafasi hiyo lakini tunashukuru kwa ushirikiano unapelekea EAC kutumiza miaka 25 ya mtangamano tangu ilivyoanzishwa 1999,” amesema.
Amesema mwaka huu jumuiya hiyo ya EAC inafikisha miaka 25 ambapo sherehe hizo zinaambatana na mkutano wa kawaida wa marais wa nchi wanachama wa EAC na kabla ya hapo kutakuwa na mikutano mbalimbali ya mawaziri, wadau mbalimbali wa sekta ikiwemo binafsi na maonyesho ya mawazi na vyakula tofauti tofauti.
Hivi sasa nafasi uenyekiti wa EAC inashikiliwa na Rais wa Suda, Salva Kiir ambaye alipokea kijiti hicho kutoka kwa Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimie
Ambapo kabla ya mkutano wa wakuu wa nchi kutatangulia vikao mbalimbali ikiwemo vya mawaziri na vikao vya juu watakaojadili mambo mengi ikiwemo uanzishwaji wa soko la pamoja,muungano wa fedha wa kisisasa na shirikisho la kisiasa ikiwemo amani na uhusiano katika ya nchi za EAC.