Mwenyekiti UVCCM Arusha achangia ujenzi nyumba ya katibu

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Simon Maxmillian ametoa Sh milioni 1 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya katibu wa umoja huo.
Fedha hizo zimetolewa leo wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara ya kamati ya utekelezaji mkoa.

Katika ziara hiyo amefanya mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kata ya Noondoto na kueleza mafanikio yanayofanywa na Rais Samia Hassan Suluhu katika kipindi cha miaka minne.



