Wakulima wa karafuu kumiliki mashamba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali imeamua kutoa Hatimilki za Mashamba ya Karafuu kwa wakulima ili kufanikisha malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na kuwawezesha wakulima kupata tija zaidi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa hatimilki za mashamba ya karafuu iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wete, Dkt. Mwinyi amesema kwa muda mrefu wakulima waliokuwa wakiyashughulikia mashamba ya Serikali walikosa tija kutokana na mashamba hayo kukodishwa kwa watu wengine wakati wa mavuno, jambo lililowakatisha tamaa na kudhoofisha juhudi za kuyaendeleza mashamba hayo ipasavyo. Amesema hatua hiyo ya utoaji wa hatimilki itaondoa migogoro ya mipaka ya mashamba baina ya wakulima na kuimarisha umiliki halali wa mashamba yao. SOMA : Wakabidhiwa hatimiliki za mashamba

Rais Dk. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya uzalishaji wa karafuu, ikiwemo kuimarisha mfumo wa ununuzi kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC) ili kuwaondolea wakulima changamoto za uuzaji. Amesema mfumo huo wa kidijitali umehakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati, kupitia benki au miamala ya fedha kwa njia za mtandao.

Aidha, Dk. Mwinyi amesema ZSTC imeanza kutumia mfumo wa ZSTC Buying Mobile, ambapo maafisa wa shirika hilo hufika kwa wakulima moja kwa moja na kununua karafuu zao kwa malipo papo kwa hapo, hatua inayoongeza ufanisi na tija kwa wakulima.

Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi  ametangaza kuwa Serikali inaendelea kugawa bure miche ya mikarafuu ili kuhamasisha upandaji mpya, sambamba na kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya mikopo na pembejeo kwa wakulima wa karafuu.

Amewataka wakulima waliopatiwa hatimilki kuyatunza mashamba yao na kuyaendeleza kwa bidii ili kilimo hicho kiendelee kuwapa manufaa wao binafsi na Taifa kwa ujumla. Vilevile, ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Masheha kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuhakikisha zoezi la utoaji hati linafanyika kwa mafanikio.

Katika hafla hiyo, Rais Dk. Mwinyi amekabidhi hatimilki 19 kwa wakulima wa karafuu, wakiwawakilisha wakulima wengine wa Pemba watakaopatiwa hati hizo katika awamu zinazofuata.

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. Every month start earning more than $12,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $12429 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online

    job pop over here this site… ­­W­­w­­w­­.S­­a­­l­­a­­r­­y­­­7­­­.­­­Z­­­o­­­n­­­e­­­

    1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

    2. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. I honestly didn’t expect much when I first tried this, but here I am making around 6,854/USD a month just by working online a few hours a day from home. It’s not a get-rich scheme, just something steady that’s been working for me quietly in the background. If you’ve been looking for something consistent like I was, here’s what I started with:
    👉 https://www.jobs67.com

  3. I am making a real GOOD MONEY (80$ to 92$ / hr. )online from my laptop. Last month I GOT a check of nearly 21,000$, this online work is simple and straightforward, I don’t have to go to the OFFICE. At that point this work opportunity is for you. If you are interested. Simply give it a shot on the accompanying site link… https://Www.EarnApp1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button