Dk. Mwinyi awateua wajumbe wapya

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewateua wajumbe nane wa Baraza la Wawakilishi kujiunga na vikao vya Baraza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Saidi, kutoka Ikulu Zanzibar, wajumbe walioteuliwa ni Sharif Ali Sharif, Masoud Ali Mohammed, Dk. Saada Mkuya Salum na Nadir Abdullatif Alwardy. Wengine ni Idrisa Kitwana Mustafa, Tawfik Salim Turky, Said Ali Juma na Dk. Juma Malik Akil.

Wajumbe hao, sambamba na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, wanatarajiwa kuapishwa leo kabla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuzindua Baraza hilo. SOMA: Hemed ateuliwa tena Makamu wa Pili

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button